Saturday, October 6, 2012

UJIO WA RICK ROSSY WA MAREKANI WAMFANYA RICK ROSSY WA BONGO "ATAMBE"


Boss wa Maybach Music Group Rick Ross jana usiku ametua nchini kwaajili ya kupiga show ya Fiesta itakayofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.

Teflon Don huyo aliwasili mida ya saa nne usiku akiwa chini ya ulinzi mkali na kupitia mlango wa VIP ambako ilikuwa vigumu kwa waandishi wa habari kupata picha zake.

Hata hivyo wakati anasuburiwa kwa hamu na mashabiki wake, alitokea mtu anayefanana na Rick Ross uwanjani hapo kiasi cha kumfanya kila mmoja amkimbilie kumpiga picha akidhani ndiye yeye.

Hata hivyo baada ya watu kugundua kuwa sio yeye bado jamaa huyo aligeuka kivutio kikubwa kwa watu wengi ambao walianza kuchukua picha zake na baadhi ya vituo vya televisheni kumhoji.

Msafara wa Rick Ross uliokuwa umezungukwa na magari ya kila aina na mabodyguard waliokuwa makini kumlinda bosi wao, uliekelea Serena Hotel ambako ndiko alikofikia.

Huko ndiko wapiga picha walifanikiwa kupata baadhi ya picha zake rapper huyo wa MMG aliyekuwa na t-shirt nyeupe na muda mwingi alikuwa busy na simu yake.
DSC_7404 (800x537)DSC_7395 (800x537)DSC_7396 (537x800)DSC_7397 (537x800)DSC_7398 (537x800)DSC_7399 (800x537)DSC_7400 (800x537)DSC_7401 (537x800)DSC_7402 (800x537)DSC_7403 (800x537)DSC_7404 (800x537)DSC_7405 (800x537)DSC_7406 (800x537)
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!