Saturday, October 13, 2012

UKICHECHE WAMPONZA ESTHER FLAVIAN......ALIKUA AKIGAWA KWA "MTITU" NA "CLOUD 112" KWA ZAMU.....

USIRI mkubwa uliokuwepo juu ya msanii wa filamu bongo Esther Flavian, kufukuzwa kwake kwenye kampuni ya filamu ya 5 Effects, inadaiwa kuwa chanzo kikubwa ni kutoka kimapenzi na Issa Musa ‘Cloud 112′ wakati huo huo akiwa kwenye mahusiano na Mtitu ambaye ndiye bosi wake.

Mwandishi wa mtandao huu
alikutana na mtu ambaye anaijua ishu hiyo kiundani bila kutaja jina lake, alidai msanii huyo awali alikuwa akifanya kazi hapo lakini alikuja kujiona yuko juu baada ya kumnasa boss Mtitu kimapenzi.

Chanzo hicho kilidai kuwa wakati akitoka kimpenzi na
Mtitu hakuna mtu aliyekuwa anajua na wakati mwingi alikuwa karibu sana na boss huyo. Baada ya muda Esther akaona haitoshi, akaamua kujiweka kwa Cloud 112.Cloud 112
baada ya kula mzingo aliamua kuweka wazi kila kitu ili watu wajue wakati akiweka wazi ishu hiyo hakujua kwamba ‘Mtitu’ naye alikuwa mpenzi wa mwanadada huyo, ndipo Mtitu alipopatwa na hasira na kuamua kumfukuza kazi Esther.

“Kumchangaya Mtitu na Cloud 112 ndiyo sababu kubwa ilimfanya afukuzwe 5Effects, na hadi leo bado anatamani kufanya kazi pale ila kwa ishu aliyofanya hawezi kurudi tena lakini wawili hao hawawekeana chuki kwani hakuna mtu aliyejua kama kila mmoja ni mpenzi wa mwanadada Esther Flavian,”
kilisema chanzo chetu.

Hata hivyo mwandishi wetu
alimtafuta Esther, ili naye aweze kuweka kauli yake ndipo alipodai kuwa habari hizo zina lengo la kuendelea kumchafua kwani mapenzi yanatokea huwa hayajifichi na kama aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kipindi cha nyuma na hao wote wawili haihusu mtu yeyote.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!