Wednesday, October 17, 2012

WAISLAM DAR NA ZENJI WAANDAMANA WAKITAKA SHEIKH PONDA AACHIWE HURU


Waislam jijini Dar es Salaam wameandamana katika maeneo ya Posta kushinikiza kuachiliwa huru kwa katibu wa jumuiya na taasisi za kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Jeshi la polisi limekabiliana na kundi la waislamu hao ambalo liliibuka muda mchache baada ya swala ya mchana na kusababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Hali hiyo imesababisha maduka yaliyo jirani na maeneo hayo kufungwa.

Polisi walimkamata Sheikh Ponda kwa madai ya uchochezi wa kidini na uvunjifu wa amani.

Kamanda kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova alitoa taarifa hiyo leo katika mazungumzo na waandishi wa habari.
Vurugu za Zanzibar

Kamanda Kova amesema Sheikh Ponda amekuwa akihamasisha maandamano yasiyo halali pamoja na kuchochea chuki na vurugu kupitia taasisi na jumuiya za kiislamu ambazo hazifuati sheria.


Ametaja tukio la kuvunjwa makanisa Mbagala Dar es Salaam Oktoba 12 kuwa nalo lilihamasishwa na sheikh huyo na wafuasi wake licha ya jeshi la polisi kuwa lilikuwa likifuatilia tukio lisilo la kimaadili.
Gari la polisi likifanya doria maeneo ya Darajani Zanzibar
Madai mengine yaliyotajwa kuwa ya kichochezi na jeshi la polisi ni pamoja na kauli ya ponda ya jana ya kuipa serikali siku saba iwaachie watuhumiwa waliochoma makanisa na kufikishwa mahakamani mapema jana jumanne.

Wakati huo huo huko Zanzibar kumetokea vurugu kubwa ya waislam baada ya Kiongozi wa kundi la Uamsho Sheikh Farid kutekwa.
Fujo za Zanzibar
Kwa mujubu wa vyanzo, Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.

Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.
Sheikh Farid ‘amepotea’ muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake (Sheikh Ponda) alikamatwa (saa 5 usiku wa kuamkia leo).
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!