Wednesday, October 3, 2012

"BAADA YA KUOKOKA, BEATRICE WA BSS AMESEMA MUDA MWINGI ANAUTUMIA KUJIFUNGIA USOMA BIBILIA


Mwanadada aliyetengeneza jina kupitia shindano la kufatuta vipaji, Bongo Star Search 2008 na 2009, Beatrice William aliamua  kuokoka siku ya juma tano tarehe 7/3/2012 katika ibada ya matendo makuu ya Mungu, katika kanisa la Mikocheni B Assemblies of God (Mlima wa moto)
Akiongea  na Mpekuzi  wetu  jana, Beatice amesisitiza kuwa  uamuzi wake wa kuokoka ni wa dhati kabisa akiwa na akili zake timamu. 

"Mara nyingi nilipenda sana  kuokoka lakini niliogopa kumbipu Mungu kama wengine wanavyofanya, "aliongea Beatrice na kuongeza

"Baada ya  kuokoka  nimekuwa  na amani zaidi  na muda  mwingi najifungia kusoma bibilia na  kuimba  kanisani bila  kujali  nalipwa nini"

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!