Thursday, October 4, 2012

"DAWA ZA KUKUZA MAKALIO ZILINIFANYA NIVIMBEVIMBE OVYO NA HIVYO NIKAAMUA KUACHA"......AUNT LULU


WAKATI wasanii wengi wa tasnia ya bongo movie wakishindwa kueleza ukweli wa mambo juu ya matumizi ya dawa za kukuza makalio na nyingi nezo wanazotumia, msanii wa filamu Lulu Mathias ‘Aunty Lulu, amekili kuwa alijaribu kutumia dawa za kuongeza makalio lakini baada ya kuona baadhi ya rafiki zake wanapata madhara aliamua kuacha.

Mwandishi wetu alimsaka hewani Aunt ili  kupata ukweli wa umbo la mwanadada huyo kama ni natural au la na baada ya kumpata, alifunguka na kudai alijaribu kutumia  dawa hizo za kukuza makalio lakini baada ya muda baadhi ya rafiki zake ambao walitumia wote walianza kupata madhara kwa kuvimba vimba hovyo kwenye makalio yao, kitu ambacho kilimpa uoga na kuacha kabisa kutumia dawa hizo ingawa aliweka wazi kuwa makalio yake ni makubwa tangu alipokuwa mdogo.

“Makalio yangu ni makubwa tangu nilipokuwa mdogo hivyo watu wanaposema kuwa nilitumia dawa za kuongeza makalio nawaona wajinga, ingawa  nilijaribu kutumia baada ya kuona madhara yake ya  kuvimba  ovyo kwa watu wengine niliamua kuacha kabisa,”
alidai.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!