Tuesday, November 20, 2012

ABDALLAH MWINYI AWASIHI WAFANYABIASHARA KUWA NA UTHUBUTU WA KUVUKA MIPAKA KAMA WAFANYAVYO WASANII


Wabunge wa EALA Abdullah Mwinyi na Shyrose Bhanji
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) na mjumbe kwa kamati ya mahesababu ya bunge hilo, Abdullah Mwinyi amesema wafanyabiashara nchini Tanzania wanatakiwa kuwa na uthubutu wa kuvuka mipaka na kufanya biashara kimataifa na kutolea mfano jinsi wasanii wa muziki Bongo Flava walivyofanikiwa kuvuka mipaka kutokana na kuthubutu kwao.


Mwinyi amesema nyimbo za wasanii wa Bongo Flava zimeteka mawimbi ya kila radio nchini kuliko muziki wa aina nyingine kwasababu wasanii wake si waoga na wamekuwa wakithubutu kufanya mambo makubwa na hivyo kuwataka wafanyabiashara kuiga mfano huo.

Akiongea na Power Breakfast ya Clouds FM asubuhi ya Jumanne hii, mbunge huyo kijana amesema kuna fursa nyingi za kibiashara katika nchi za Afrika Mashariki ambazo wafanyabiashara wa Tanzania wanatakiwa kuzichangamkia.

Katika kipindi hicho wamemtolea mfano Ambwene Yessaya aka AY ambaye weekend iliyopita aliitoa kimasomaso Tanzania kwa kunyakua tuzo ya Channel O katika kipengele cha video bora ya wimbo wa Afrika Mashariki ngoma yake ‘I don’t wanna be Alone aliowashirikisha Sauti Sol wa Kenya.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!