Tuesday, November 27, 2012

BARNABA AZIDI KUANDAMWA NA MIKOSI......


Msanii Barnaba Elias ameendelea kuandamwa na mfululizo wa mikosi, baada ya wikiendi iliyopita kuibiwa gitaa lake ambalo alipewa na Mke wa Rais wa Marekani aliyopita Mama Laura Bush. Barnaba alielezea kusikitishwa na tukio hilo ambapo anasema liliibwa maeneo ya Leaders nje ya ofisi za THT ambapo ndipo makao makuu ya kituo chao cha kazi.

Akiongea na paparazzi wetu Barnaba alisema, baada ya kuingia katika ofisi za THT siku ya jumamosi, majira ya saa kumi na kumi na mbili na kufanya mambo yake, alishangaa kutolikuta gitaa lake hilo alilopewa kama prize Asset na Laura Bush, Mke wa Rais aliyepita na alichanganyikiwa kidogo kwa namna lilivyotoweka.


“Ninavyokwambia nilifunga milango yote lakini hawa jamaa wametumia mbinu kali maana hakuna mtu aliyeshituka. "


Barnaba anasema bado juhudi za kulitafuta gitaa hilo zinaendelea na anasema atashukuru kama atapata mtu atakayemsaidia kwa taarifa ili kulipata gitaa hilo
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!