Wednesday, November 7, 2012

JACK WOLPER NA IZZO B NDANI YA FILAM MOJA ..."MY PRINCES"


MKALI wa Bongo Fleva, Emmanuel Simwinga ‘Izzo B’, ametanuka kisanii na sasa ametupa kete yake nyingine kwenye filamu ya My Princess aliyocheza na mrembo mwenye mvuto wa kipekee,  Jacqueline Wolper Massawe .

Akizungumza na mwandishi wetu, Izzo B alisema, yeye ni msanii mwenye vipaji vingi na huu ni wakati wake kuonesha Watanzania kuwa hata kuigiza yupo poa.

“Huu ni mwanzo tu, baada ya hii nitakuja na vitu vikali zaidi. Natamani sana mashabiki wangu waone kazi niliyoifanya, najua watanikubali tu. Sijabahatisha, niko vizuri ndiyo maana nimeona nijaribu na upande wa pili kama wanavyofanya wasanii wa mamtoni,” alisema Izzo B.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!