Thursday, November 1, 2012

JAMILA AKANA KUWA YEYE SIYO HOUSE GIRL WA WEMA SEPETU

MWANADAFADA aliyezaa na msanii wa Bongo Fleva, Amani Temba kutoka TMK Wanaume, Jamila Msafiri amefunguka kuwa anakerwa sana na tabia ya baadhi ya watu kumpakazia kuwa yeye ni hausigeli wa Wema Sepetu kutokana na ukaribu walionao wawili hao

Wema Sepetu.
Akichonga na Mpekuzi, Jamila alisema Wema ni rafiki yake kama walivyo marafiki wengine na kutaka watu waache kutafsiri tofauti kwani wanamkosesha raha.

“ Kwa nini mtu anapokuwa karibu na Wema wanampachika majina ya ajabu ajabu? Hata Snura naye walimpachika majina ya ajabu, kwani Wema hawezi kuwa na rafiki? Hata Obama ana marafiki sembuse Wema,” alisema Jamila.Jamila Msafiri.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!