Thursday, November 1, 2012

JOH MAKINI ACHUKIZWA NA KITENDO CHA WASANII WA ARUSHA KUTOSHIRIKISHWA KATIKA UZINDUZI WA JIJI HILOMweusi Joh Makini ameungana na wasanii wengine wa Arusha waliochukizwa na kitendo cha wasanii wa Arusha kutoshirikishwa kwenye sherehe za kulizindua jiji hilo rasmi.

Joh ambaye huandika mara chache kwenye ukurasa wake wa Facebook ameandika, “Arusha inakua jiji leo huku wasanii wa arusha ambao muziki wetu umekua ukiitangaza nje na ndani ya nchi hatuhusishwi wala kupewa heshima tunayostahili,mweusi.”


Awali Muungano wa wasanii wa muziki Arusha, ukiongozwa na wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Nakaaya Sumari na Chindo Man waliuijia juu uongozi wa Jiji la Arusha kwa kumwalika Diamond katika uzinduzi wa jiji hilo na wao kutelekezwa.

Wasanii hao wanadai kitendo kilichofanywa na waandaaji wa shughuli hiyo kumwalika Diamond na kuwaacha wasanii wa Arusha katika sherehe hizo ni dharau kubwa kwao.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!