Thursday, November 15, 2012

LADY JAYDEE ATAMBUISHA RASMI KIPINDI HAKE CHA "DIARY"

 LADY JAYDEE
  Mkurugenzi wa Machozi Band,  Lady Jaydee akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salalaam leo wakati wa uzinduzi wa kipindi chake cha 'Diary Ya Lady Jaydee' kitakachoanza kurushwa hewani kila siku ya Jumapili kupitia televisheni ya EATV. Kushoto ni Mkuu wa Vipindi EATV, Lydia Igarabuza.

Mkuu wa vipindi wa Televisheni ya EATV, Lydia Karabuza akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kipindi cha televisheni cha 'Diary Ya Lady Jaydee kitakachoanza kurushwa hewani kuanzia Jumapili.
-------------------------------------------
Lady Jaydee akiongea na waandishi wa habari
Msanii nguli wa kike ambaye ana majina mengi kama Komando, Jide, Mama Some food n. k leo asubuhi ameongea na waandishi wa habari na kutoa taarifa rasmi kwenda kwa watanzania juu ya ujio wa kipindi chake kipya cha TV kitakachoitwa “Diary ya Lady Jaydee”.


Msanii huyo wa kike ambaye kwa sasa anatamba kwa hit song yake ya ya “ Mimi Ni Mimi” alisema kipindi hicho cha Diary ya Lady Jaydee kitazungumzia maisha yake kwa undani kikitazama mambo kama njia aliyopitia kufanikiwa, mahusuiano yake binafsi na mwandani wake pamoja na washkaji,wadau na ndugu jamaa na marafiki, ikiangalia pia namna alivyoweza na anavyokabiliana changamoto mbali mbali, mipango yake ya kimuziki, maisha na biashara.

Naye mkuu wa vipindi katika kituo cha televisheni cha East Africa TV Lidya Igarabuza alisema katika kipindi hicho kitakachokuwa kikiruka siku ya kila Jumapili ya wikiendi hii na kuendelea kitakuwa kikionekana kuanzia mida ya saa 3 usiku na kuonekana kwa nusu saa tu.


Akiendelea Lidya alisema wao kama kituo namba moja cha TV kwa vijana wamechukua fursa ya kukubali kuonyesha kipindi hicho cha Diary ya Lady Jaydee kwa sababu Jaydee msanii mkubwa tu Tanzania bali Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na hivyo kwa sababu ana mashabiki wengi ni faraja kubwa kwa kituo hicho kuongeza idadi ya watazamaji ambao ni wapenzi wa msanii huyo.

Akimalizia mkuu huyo wa vipindi alisema kipindi hicho kitakuwa na episode 52 kwa maana kipindi kimoja kwa wiki kwa mwaka mzima hivyo kuwataka watazamaji wa TV hiyo kukaa mkao wa kula wakisubiri kuona ni nini kitaonekana kuanzia jumapili hii.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!