Monday, November 12, 2012

MABANGO YENYE USO WA RIHANNA ULIOJERUHIWA MWAKA 2009 YATUMIKA KUIPINGA SHOW YA CHRISS BROWN HUKO SWEDENRihanna anaweza kuwa ameshamsamehe Chris Brown kwa kumpiga miaka mitatu iliyopita lakini kuna watu mjini Stockholm, Sweden bado hawajamsamehe.

Kwa mujibu wa website moja ya nchini Sweden, Alour se, mabango yenye picha ya mpenzi wake wa zamani na Chris zinazoonesha alivyojeruhiwa usoni kutokana na kipigo hicho yamebandikwa kwenye mitaa kadhaa mjini humo kupinga show yake ya November 19.


Chris bado yupo kwenye probation kwa miaka miwili mingine kutokana na kumpiga vibaya Rihanna mwaka 2009. Chris na Rihanna hivi karibuni wamerudisha urafiki wao kiasi cha Breezy kumpiga chini mpenzi wake Karrueche Tran ili tu kuwa karibu na muimbaji huyo wa Diamonds.

Kwa mujibu wa interview ya hivi karibuni kupitia Facebook Live Chat na Andy Cohen Rihanna alisema hana uhusiano wa kimapenzi na Chris.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!