Monday, November 19, 2012

MAKALA:CHAZO CHA MVUTANO KATI YA TANZANIA NA MALAWININAPO TAMANI KUONA SULUHU YA ZIWA NYASA

Kumekua na mvutano kati ya Tanzania na Malawi unao sababishwa na mpaka katika Zawa Nyasa.Historia inaonyesha kuwa mvutano huo ualianza mala tu baada ya Uhuru wa Malawi  mwaka 1964 ambapo wakati huo ikijulikana kama Nyasaland. Ikumbukwe kwamba Candido Jose da Costa Cardoso mfanya biashara mkubwa na maarufu wa kireno wakati huo ndie mtu wa kwanza kufika (kuligundua) Ziwa Nyasa mwaka 1846 kabla ya David Living Stone ambae alifanikwa kufika mwaka 1859, na baadae Muingereza kuzitawala nchi zinazo lizinguka Ziwa hilo na kuitwa Nyasaland. Mvutano huo umechukua sura mpya hivi karibuni baada ya serikali ya Malawi kusema kwamba Ziwa lote ni mali yao, hali hiyo ilisababisha waziri wa mambo ya nje na ushiriano wa kimataifa wa Tanzania, Benard Membe kusema Tanzania ipotayari kwa lolote katika kutetea ziwa Nyasa .Alitoa msimamo huo bugeni wakati akisoma hotuba ya wizara yake tarehe 06/08/2012 (jumatatu)na kuitaka Malawi kufanya mazungumzo na Tanzania,lakini ikumbukwe kwamba tarehe 04/08/2012, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi,Ephraime Chiume alisikika akisema kwamba, kwa mujibu wa mkataba wa mwaka 1890(Heligoland Teaty) ambao ulisainiwa kati ya Uingereza na Ujerumani unawapa malawi umiliki wa Ziwa hilo, alisisitiza kwamba hata Maazimio ya Umoja wa Afrika yanatambua ziwa hilo ni lao.

Tanzania ilipata habari kupitia shirika la TPDC (Shirika la Taifa la maendeleo ya petrol)kua eneo lote la Ziwa Nyasa,kaskazini mwa Msumbiji limegawanywa kwenye vitalu,na kwamba serikali ya Malawi imetoa vitalu hivyo kwa kampuni ya utafiti wa mafuta na gesi,Serikali ilikua na ushahidi kwamba ndege ndogo za utafiti zenye uwezo wakutua majini na ufukweni zinazokadiriwa kua tano zilionekana zikivinjari katika eneo la Ziwa Nyasa upande wa Tanzania kati ya January 29 na Julai 2,mwaka huu(mwaka 2012)licha ya kunyimwa kibali na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Hali hiyo ilisababisha serikali ya Tanzania kuitaka Malawi kutoruhusu mtu au kampuni yoyote ile kuendelea na shughuli za utafiti kwenye eneo lote linalobishaniwa, serakali ya Tanzania iliamua kuimalisha ulinza katika Ziwa Nyasa hali ambayo ilisababisha hofu kwa Malawi wakijua kwamba mapigano yatatokea baada ya ulinzi unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa lengo la kudhibiti vitendo vya uchokozi kutoka Malawi.CHAZO CHA MVUTANO KATI YA TANZANIA NA MALAWI

Baada ya uhuru wa Malawi mwaka 1964 serikali ya nchi hiyo imekua ikidai na kuamini kwamba mpaka wetu na wao kwenye Ziwa Nyasa unapita pwani na kwa maana hiyo Ziwa lote la Nyasa kutoka kwenye mpaka wa msumbiji( Mozambique) hadi Malawa ni mali yao.wanadai kwamba mkataba uliowekwa saini kati ya waingereza na wajerumani mwaka 1890 uliweka mpaka kwenye pwani au ufukwe wa Ziwa Nyasa mkataba huo unajulikana kama Heligoland treaty or Anglo- German Agreement.

Kwa upande wa Tanzania, tunadai kwamba mpaka kati yetu na Malawi kwa Ziwa Nyasa unapita katikati ya Ziwa hilo,kutoka pale Malawi na Msumbiji (Mozambique) wanapopakana, usawa wa Nyuzi 11 Kusini hadi mwisho wa Ziwa kule Kyela kwenye digrii 9 kati ya Ziwa, kwa madai kwamba Nyaraka na ramani zilizo tengenezwa na wakoloni wetu mwaka 1928,1937 na mwaka 1939 zinaonyesha kuwa mpaka wa Ziwa hilo upo katikati.

Mwaka 1967 kulikua na vita kali ya maneno ( A serious war of words) kati yetu na Malawi, hali iliyo sababisha mpaka kushikishana adamu kidogo katika maji ya Ziwa Nyasa baina yetu na Malawi kutokana na uhusiana mbaya uliokuwepo wakati huo kati ya Rais Julius Nyerere na Hastings Kamuzu Banda wa Malawi wakati huo, hii ni kutokana na Rais Hastings Kamuzu Banda Kuunga mkono Serikali ya kikaburu nchini South Africa ambayo mwalimu Nyerere alikua haungi mkono.

TANZANIA IZINGATIE YAFUATAYO KATIKA MZOZO HUU

Tuwe wamoja katika kupambana na Malawi, serikali lazima ihakikishe kwamba wa Tanzania wote tunakua wamoja katika kipindi hiki cha mzozo wa Ziwa Nyasa, huu si wakati wakuleta mpasuko wa kisiasa, ikumbukwe kwamba Rais  wa Malwai Joyce Banda amesha kutana na viongozi wa vyama vya upinzani akiwataka kuwa wamoja katika kupigania nchi yao. Hivyo basi wa Tanzania lazima tutambue kwamba katika mgogoro huu tunazidisha umoja ili tuweze kuisaidia serikali yetu, niombe serikali ikutane na wadau tofauti katika kuhakikisha tunajipanga kuikabili Malawi.

Tusi idharau Malawi, Serikali na Watanzania kwa ujumla wetu hatupaswi kuitazama Malawi kama nchi dhaifu na isiyo weza kufanya jambo lolote kwetu,  adui dhaifu anaweza akafanya maajabu na kuishagaza dunia( We don’t need to underestimate our enemy). Lazima tutambue kwamba katika mzozo kama huu adui nae anatafuta mbinu za kutushinda, hivyo basi lazima tujipange kwa lolote litakalo tokea lakini tusidharau  Malawi.Lazima tujue wana hoja gani na sisi tunahoja gani halafu tunapigana vipi, tuache propaganda zisizo na msingi katika kulindi maslahi ya nchi yetu nasio kuwaona Malawi kama wadhaifu wasio na mipango na nguvu katika kupigania Ziwa Nyasa.Tujiulize nguvu ya chokochoko hizi zimetoka wapi? Kama wao ni dhaifu vipi wame kuwa manunda katika hili,hivyo basi laziwe tuwe wakali katika kutetea Ziwa Nyasa bila ya kuona Malawi kama nchi dhaifu.

Tukumbuke mzozo wa Kagera,watanzania lazima tukumbuke vita vya kagera mwaka 1978 hadi 1979 pamoja na chuki, uadui na uhasama kati ya Mwalimu Nyerere na Iddi Ammin Dada, baada ya Uganda kudai kwamba mpaka wa nchi hizi mbili ni mto kagera na kusababisha kuvamiwa kwa kaskazini magharibu( Bukoba) mawa Tanzania Octoba 30,1978 na kutekwa kwa eneo kubwa la nchi yetu hali ambayo ilitughalimu kulikomboa. Hivyo basi hatakama tuna nguvu ya kuipiga Malawi kivita hatu paswi kukimbilia katika suala hilo kwani tukikurupuka itatu gharimu kama ilivyo kuwa kwa Iddi Ammin Dada.Licha ya Iddi Ammin Dada kuondolewa Novemba 25,1978 na April 11, 1979 adui kuikimbia Uganda lakini Tanzania ilidhohofika sana, kwa mfano uchumi wetu ulizorota na kuyumba vibaya sana pamoja na ulemavu wa kudumu ambao wazalendo waliokuwa wakikomboa nchi yetu waliupata. Je tumejipanga na kufikiria haya kabla ya kusema Tanzania ipo tayari kwa lolote?

Tukusanye ushahidi wa kutosha ilituwe na vielelezo thabiti vya kuishinda Malawi, Serikali lazima ipitie nyaraka muhumu kwa kufanya uchambuzi makini( cross-examination) wa nyaraka mbalimbali mbazo zipo, tusiwe wepesi wa kufanya maamuzi bila ya kuwa na uthibitisho katika mambo nyeti kama haya( A delicate diplomatic matters of the state). Tuwe na uthibitisho sahihi kwa kusoma nyaraka zote , zile zinazo semekana ni za kweli na zile zinazo lalamikiwa kutokakna na mapungufu ili tujilidhishe na tuwe wenye kujiamini tunapo tetea Ziwa Nyasa letu.

Malawi ni kibaraka wa nchi za kigeni,Watanzania kuna kila sababu ya kukubali na kuamini kwamba Rais Joyce Banda na serikali yake ni vibaraka wa nchi za kigeni hivyo basi hata katika mzozo wa ziwa nyasa inawezekana akawa anasukumwa na nchi hizo, kwa mfano serikali ya Malawi imekubaki ndoa ya jinsia moja ili kuendana na matakwa ya wahisani wa kigeni kama uingereza kwa kisingizio kwamba misaada kutoka uingereza itasaidia kutatua tatizo la umasikini.  Swali ni je serikali gani duniani ambayo inaweza kujikwamua na umasikini kwa kutegemea misaada tena yenye mashariti, Kwanini wahisani hao wasitowe misaada bilaya mashariti kama kweli wanaipenda Malawi, Je serikali ya Malawi inasindwa kujua hili?. Kitu kigine ni pale serikali ya Rais Joyce Banda kukwepa kua mwenyeji wa mkutano wa Afrika iki hofu kwamba Rais Ommar Al-Bashir wa  Sudani angeuzuria hivyo basi serikali yake ingekosa misaada kutoka nchi wahisani, ukizingatia hayo kuna uwezekana Rais Joyce Banba akatumiwa na nchi za kigeni ili alete chokochoko katika Ziwa Nyasa akilubuniwa kwa misaada . kuna mambo mengi yana semwa, wengine wana amini kwamba Malawi anapewa jeuri na Muingereza kwani hata kampuni iliyo pewa leseni ya kutafiti gesi na mafuta ni ya Uingereza ijulikanayo kama SURESTREAM hivyo basi tusi pandishe jaziba bila ya kujua nyuma ya pazia kunanini. Lengo si kuogopa eti Malawi anasaidiwa nanani bali ni kutaka kutafuta njia madhubuti ya kumshinda kwa lolote litakalo tokea.

Serikali ikumbuke yaliyo tokea miaka ya sitini (1960s), katika kipindi hiko Rais wa Malawi Hastings Kamuzu Banda na Mwalimu Nyerere wa Tanzania walishindwa kupata suluhu ya tatizo kuhusu hata jina tu la Ziwa hilo, je tuna hoja gani mpya ukiacha zile za mwalimu Nyerere ambazo zilishindwa kuzaa matunda. Ilifika wakati Rais Hastings Kamuzu Banda alisikika akidai kuwa maeneo ya Songea, Kyela na Njombe yalikua sehemu ya nchi ya Malawi,alikua akidai ya kwamba alipatiwa kumbukumbu(Ramani) na Baba yake, hali hiyo ilitaka kusababisha vita kali kati ya Tanzania na Malawi mwaka 1968.

Mkataba ambao Malawi wanautumia kama nyenzo ulikua na lengo la kuonyesha kwamba nchi hiyo ilikua nchini ya Uingereza na Tanzania chini ya Ujerumani, Nimekua nikishangazwa na Serikali ya Malawi kukosa  umakini katika mzozo wa Ziwa Nyasa, mfano ni pale wanapo jichanganya katika kutumia Azimio la Umoja wa Afrika la mwaka 1963,linalo taka nchi wanachama wa Africa kukubaliana na mipaka iliyopo, hili si jambo baya lakini wakumbuke kwamba katika ibara ya sita ya Heligoland  Treaty wa 1890  ambao ni msingi wa madai yao unabainisha kwamba nchi zinazo husika zikutane na kurekebisha kasaro katika mazingira yatakayo lazimu, je wamalawi hawalijui hili au kwa nini hawalisemi hili?, waache kutumia Azimio la Afrika la mwaka 1963, na 2002,2007 ilihali wakiwa hawa zingatii ibara ya sita ya mkataba( section six of Heligoland Treaty/ Anglo-German Agreement) wa mwaka 1890. Ninge penda serikali iwaulize Malawi hivi kweli mkataba huo ulikua halali kwa Tanzania?( Was it legitimate?) kwa sababu Tanzania( Tanganyika before the Indepence) haikushiliki katika kuandikwa kwa mkataba huo wa mwaka 1890.

Mzozo kama huu si wa kwanza kutokea dunian,Tanzania haipaswi kuyumba katika mzozo huu kwani isha wai kutokea sehemu mbalimbali za dunia, mfano safi ni hapahapa barani Afrika baina ya CAMEROON na NIGERIA kuhusu mpaka wao katika ziwa chad katikati ya Nigeria na Cameroon, baada ya kushindwa kupata suluhisho wali kwenda kwenye mahakama kuu ya Dunia, na hivyo basi ika amuliwa mpaka upite katikati ya Ziwa Chad ukifuata msitari ulio nyooka (A median Line). Dunia inatambua kwa nchi mbili zinazo tenganishwa na maji mpaka wake ni katikati ( Where there is shared water body the border is at the middle) ikimaanisha zina tenganishwa na msitari ulio nyooka ujulikanao kama MEDIAN LINE. Kwa kuzingatia mfano huo na mingine duniani serikali yetu lazima ijipange madhubuti kuishinda Malawi, Historia inaonyesha kwamba hakuna ‘’case’’ ( mgogoro) kama huu duniani ambao umme amuliwa kwa kwa nchi moja kupewa Ziwa au Mto wote kitaalamu ijulikana kama ( One hundred percent monopoly) bali, suluhisho utolewa kwa kwa kuangalia asilimia hamsini, kitaalamu ujulikana kama (Fifty percent solution)

Kama tutakwenda mahakama ya dunia tuzingatie vigezo muhimu, kuna vitu muhimu ambavyo mahakama ya dunia inazingatia katika mizozo kama huu wa Ziwa Nyasa, kwanza serikali husika lazima iwe na takwimu sahihi( correct details) kutoka kwa wakazi wa eneo husika na vyanzo vingine, hivyo basi lazima serikali ipate taarifa kutoka kwa watu wanaolizinguka Ziwa Nyasa kwa Upande wa Tanzania ili waweze kutoa uthibitisho utakao saidia kupambana na Malawi.Kingine ni kwamba Serikali lazima itambue na isimamie ya kwamba Mkataba wa mwaka 1890( Heligoland Treaty/ Anglo-Germany Treaty)  ulikiuka sheria na mila za kimataifa,kitaalamu inajulikana kama( Customary International law) kwa sababu hauku zingatia haki za wakazi wa eneo hilo, kama vile tamaduni zao na maisha ya kila siku. Haya yote yanatosha kuipiku Malawi katika kulipigania Ziwa Nyasa.

Tusisahau kuwakumbusha Malawi mambo haya,Serikali yetu lazima itowe taarifa kwamba mwaka 1928 wakati wa utawala wa Donald Cameroon ambae alikua Gavana wa pili wa Tanganyika, alikutana na Gavana wa Nyasaland ili kubadilisha mpaka wa nchi hizi mbili na kuwawezesha wakazi wa pande mbili kutumia Ziwa Nyasa bila tatizo, swala hilo halikuzingatia mkaba wa mwaka 1890 ambao ulikua na lengo la kuizuia Ujerumani kutotumia Ziwa Nyasa na sio kuwapo kwa mpaka kati ya Tanganyika na Nyasaland, hivyo basi kwa kuwa mjeruman alinyang’anywa Tanganyika na kuwa  kwenye himaya ya muingereza kama ilivyokuwa kwa Nyasaland(Malawi) magavana hao walikubaliana mpaka upite katikati ya Ziwa Nyasa kwakua nchi zote mbili zilikua kwenye utawala wa muingereza.

Tusiwe watumwa wa nchi za kigeni kutoka Asia au Amerika, Tanzani lazima itambue umuhimu wa mipaka yetu, isitokee nchi yoyote iwaka inataka tutuingilia katika maamuzi ya nchi yetu, tusikilize ushauri wao lakini wasiwe na lengo na kutaka kufanikisha masilahi yao, dunia sasa ipo katika vita ya kutafuta mafuta na nishati nyingine kama gasi ( Oil imperialism) inayo ratibiwa na Nchi kubwa duniani kama vile Uingereza na Marekani pamoja na Zile Zinazokuwa kwa kasi kiuchumi. Kama wakijuwa Ziwa Nyasa kuna hivyo vitu(Mafuta na Gesi), wanaweza kuvaa ngozi ya kondoo wakati wao ni chui kwa lengo la kufanikisha mahitaji yao, Swala hapa ni mpaka kati yetu na Malawi, kwani Tanzania inahaki kama nchi nyingine kulinda mipaka yake bila ya kujali kama kuna mafuta na gesi au la,lazima tuijulishe Malawi na dunia yote  kwamba, tunapigania Ziwa Nyasa si kwa sababu ya mafuta au gesi bali ni mpaka wetu ambao ni muhimu kwa maendeleo na amani ya nchi yetu.Mwandishi mjoja wa maswala ya mipaka JEAN BLANCHARD aliwai kusema hivi, ‘Boundaries are external assets to surmount domestic deficiencies’’ hivyo basi kulinda na kupigania mipaka yetu haisababishwi na kuwapo kwa mafuta au gesi.Malawi lazima itambue kwamba atakama ikitokea sehemu nyingine tutapigania mpaka wetu bila ya kujali kuna nini,kama swala la gesi Malawi itambue kuwa, Mnazi bay, songosongo na maeneo ya Zanzibar kumegundulika gesi nyingi sana ambayo wao hawana hata theluthi yake, swala letu na wao ni mpaka. Watanzania wapatao laki sita 600,000waliopo eneo hilo wanapaswa kulitumia Ziwa Nyasa kwa kuamini kwamba Ziwa hilo ni Triple heritage, ambapo wakazi wa Msumbiji, Malawi na Tanzania limekuwa zawadi kwao kwani limewazunguka kila mmoja, hali inayosababisa mpaka wake uwe katikati ya ziwa hilo.

Imeandaliwa na Suleman A Kuchengo
Mwanafunzi mwaka wa tatu,
Digrii ya Uhusiano wakimataifa(International Relations).
Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
0714937641/suleykuchengo@yahoo.com
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!