Thursday, November 22, 2012

MAMBA AUA MWANAFUNZI NAKUJERUHI BABA MWANZA

 MWANAFUNZI mmoja Pascal Abudallah (14), wa Shule ya Msingi Nantare ameuawa na mamba kijijini hapo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Ngoma, Mwanza vijijini, Khamisi Ndaro amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na akaongeza kwamba kilitokea saa 1.30 usiku mwishoni mwa wiki iliyopita na tayari mtoto amezikwa kijijini hapo.


Aliongeza kuwa licha ya kifo cha mtoto huyo, baba mmoja aitwaye Mtimba Manyeye (64) naye alipoteza kidole cha mkono wa kushoto baada ya kushambuliwa na mamba akiwa kando ya Ziwa Victoria.


Aidha, Afisa Mtendaji Ndaro alisema wanyamapori wamekuwa wakisumbua wananchi na akatoa mfano wa nyani ambao wapo zaidi ya 1,000 nao wamekuwa  wakisumbua sana wakulima wa eneo hilo kwani wameharibu zaidi ya hekari 150 za mashamba yao, hivyo kuwafanya kukata tamaa kuendelea kulima.


“Maofisa wa wanyamapori wamekuwa wakifanya msako lakini wanyama hao wanaendelea kuwa tishio kwa raia,” alisema Ndaro.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!