Thursday, November 1, 2012

MBUNGE WA CCM AMWACHIA LAANA BINTI YAKE


Binti alipofumaniwa
--------------------
KATIKA hali inayoonekana ni kukerwa na kitendo cha bintiye Naima Shah kuonekana kwenye magazeti akiwa katika picha chafu, Mbunge wa CCM amemtoa mwanawe huyo kwenye orodha ya warithi wake endapo atatangulia mbele za haki.


Akizungumza na mwandisi wetu juzikati jijini Dar, binti huyo alikiri kuwa baba yake alikerwa na picha zake na kusema hahitaji hata kumwona, akifa asifike kushuhudia mazishi yake na kwenye mirathi hayumo.
 Binti alipofumaniwa
------------------------------
“Nimeumia sana kwa kauli alizonitolea baba, sikutegemea kama hali hii ingefikia huko. Kinachoniuma zaidi, si kurithi mali zake bali kitendo cha kukosa radhi yake.

“Hivi ninavyoongea na wewe mwandishi, baba hataki kuniona machoni au kunisikia, naomba nitumie nafasi hii kuomba radhi kwenye familia yangu pamoja na upande wa mume wangu kwani nakiri sikutenda haki,” alisema Naima ambaye anaonekana kwenye video ya Wimbo wa Mbagala wa msanii Diamond.

Ijumaa iliyopita, gazeti moja la udaku lilitoka na habari ya Naima ikiwa na kichwa kisemacho: UFUSKA ikiambatana na picha chafu za binti huyo ambaye pia ni mke wa mtoto wa mfanyabiashara maarufu nchini.


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!