Wednesday, November 21, 2012

ROSE NDAUKA UFUNGUKA KUHUSU SKENDO ZA UTAPELI ZINAZOMKABILI

Habari mpya  kutoka kwa Rose Ndauka baada ya  kupiga story na mwandishi wa habari hii  ni  kuhusu skendo za utapeli.....

Mrembo  huyu amefunguka  na   kusema kwamba kumekuwa na madai mengi sana kwamba amekuwa akiitisha usahili  kwa wasanii chipukizi na kuwachukulia fedha bila kuwashirikisha katika filamu zake.....

Ndauka alikanusha na kusema kwamba sio habari za kweli kwani anapoita usahili pale mtu anapofanya vizuri anamchukua na kama akifanya vibaya basi anamuelekeza ili siku nyingine atakapoitaji tena aweze kushiriki tena. 

Hayo ndiyo maneno ya Rose Ndauka baada ya kuchonga nasi  kuhusiana na tetesi ambazo zilikuwa zikizungumziwa kwamba anawachukia wasanii chipukizi wa filamu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!