Saturday, November 24, 2012

SHILOLE ANUSURIKA KUKAMATWA NA POLISI BAADA YA KUHISIWA KUWA ANA MISOKOTO YA BANGI


MSANII wa anayefanya vizuri kwenye muziki na filamu Shilole, amenusurika kumakatwa na polisi baada ya kuhisiwa kuwa na misokoto ya bangi ndani ya gari lake na kusababisha kuhojiwa kwa dakika kadhaa maeneo ya Kinondoni.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo msanii huyo inadaiwa alikuwa akitokea kwenye ishu zake ndipo maafande hao wanaliokuwa wakitokea kwenye malindo yao walipomdaka na kumpeleka pembeni kwa lengo la kufanya upekuzi kwenye gari yake.


Inadaiwa kuwa polisi hao hawakukuta kitu chochote zaidi ya sigara za mpenzi wake, ambaye walikuwa wote usiku huo na hata hivyo hawakuwa na dalili zozote za kuwa wamelewa.


Shilole
alipozungumza na mwandishi wetu alidai kuwa tukio hilo lilimshangaza sana kwani hakuwa na bangi ndani ya gari lake na hajawahi kutumia kitu hiyo lakini polisi hao walimuhoji kana kwamba anatumia bangi.

Alidai kuwa kuna baadhi ya watu walitaka kumfanyia mchezo mchafu lakini walishindwa kwani alikuwa makini katika kila jambo ambalo alikuwa akilifanya usiku huo, na alipoulizwa kuwa usiku huo alikuwa anatoka wapi alidai kuwa katika harakati zake za hapa na pale.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!