Saturday, November 24, 2012

SIMU YASABABISHA APEWE KIPIGO CHA MBWA MWITU.......


Bi Pendo akihojiwa na waandishi wa habari

Bi Pendo Malima (31) mkazi wa Buhare Musoma Mkoani Mara ni moja kati ya wanawake waliokumbwa na tatizo la domestic violence mkoani humo, ambapo kutokana na kutokuwa na imani na mawasiliano anayoyafanya kwa kutumia simu ya mkononi mumewe alimpa kipigo kikali hadi kufikia hatua ya kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara huku hali yake ikiwa mbaya na kichwa chake kinatingishika kutokana na vipigo anavyopata, kisa simu ya mkononi!

Kwa mujibu wa blog ya ‘mwanawaafrika’, Bi Pendo aliwaambia waandishi wa habari ambao walimtembelea hospitalini hapo kuwa mumewe anaefahamika kwa jina la Ndege Aloyce humpa kipigo mara kwa mara, lakini ilifikia hatua akamfungulia dozi ya kipigo yaani mara tatu kwa mwezi hadi kufikia hatua ya kuzoea dozi hiyo na kuona ni kawaida tu.

Hata hivyo Bi Pendo ambae ni mama wa watoto watatu wa mumewe huyo anaefanya kazi ya uvuvi alisema atakapopona hatarudi tena kwa mumewe akiogopa kugeuzwa punching bag. Hii inamaanisha anachotaka kufanya bi Pendo nikuiacha ndoa yake na kuishi maisha yake bila kurudi kwa mumewe tena pindi tu atakapotoka hospitalini hapo.

Lakini hii inaonesha kuwa atazidi kunyanyasika kwa sababu hajui sheria inasema nini na itamsaidia vipi kupata haki yake kutoka kwa mumewe huyo mgawa dozi ya kipigo. Duh, wanaharakati wa maswala ya kijinsia mna kazi ya ziada huko Mara na mikoa mingine.

Japokuwa hurahisisha mawasiliano, ujio wa simu za mkononi hasa huku kusini mwa jangwa la Sahara kumekuja na changamoto nyingi sana hasa kwa watu walio kwenye mahusiano ya kimapenzi na ndoa kwa kutaka ku monitor simu za wenzi wao kwa kutokuwa na imani na mawasiliano yao.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!