Monday, November 5, 2012

TOILET PAPER ZENYE SURA YA OBAMA ZASAMBAA KWA KASI FLORIDA FIRE STATION

Yakiwa yamebaki masaa machache wananchi wa Marekani waanze kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo kwa awamu nyingine, visa na mikasa ama vituko vimezidi kutawala katika kampeni za uchaguzi huo labda ni mzuka wa kuonesha hisia za watu tofauti tofauti kwa yule wanaemsapoti na kumponda wasiyemsapoti.

Hivi karibuni watu wanaosadikika kuwa ni wapinzani wa rais Obama wametoa toilet paper zenye sura yake na T.P hizo zikasambaa maeneo ya firestation huko Florida.

Ripoti zinasema toilet paper hizo zimetolewa kujibu mashambulizi baada ya mfanyakazi mmoja wa kituo hicho cha zimamoto aliziondoa sticker zote zinazompinga Obama ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye maeneo ya umma na sio maeneo ya watu binafsi ama mali binafsi.

Hata hivyo toilet paper hizo nazo zimeondelewa maeneo hayo na kupigwa marufuku maeneo hayo ya Florida firestation kwa sababu ni maeneo ya umma (public place) na sio maeneo binafsi.

Hivi karibuni zilisambaa T-shirt zenye maneno ya kumpinga mpinzani wa Barack Obama katika kinyang’anyiro hicho cha urais wa taifa kubwa duniani Mitt Romney, t-shirt hizo zilizotengenezwa na vizuri kwa ushirikiano wa madesigner watatu John Searles, Aaron Rhodan na Julian Streete zina maandishi yanayosomeka, “That Mitt I Don’t Like.”

Siku ya jumanne November 6, ikiwa na maana kwamba ni masaa machache tu kuanzia sasa raia wa Marekani watapiga kura kumchagua rais wa tiaifa hilo na hapo ndipo maoni ya wengi yatashinda. Ni Romney ama ni Obama tena? 
 
Kura ndiyo muamuzi wa mwisho, hizi nyingine za kutoleana T-shirt na kuwekana kwenye toilet paper ni mbwembwe tu na mizuka ya baadhi ya watu ili kushawishi watu wengine kujiunga nao na kufata maoni yao.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!