Saturday, November 10, 2012

WALTER CHILAMBO NDO MSHINDI WA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012

Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri  (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar)
Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi wa shindano hilo,lililofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,usiku huu.
Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi
Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na jaji mkuu wa Shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), akiwa amemkumbatia mshindi wa shindano hilo Walter Chilambo usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond,Chilamba ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 50
Msanii Barnaba akiimba na mmoja wa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),
Mshiriki wa EBSS NshomaNg'hangasamala akiimba moja ya wimbo wake jukwaani.
Mwanadada Salma Albushiri akiimba kwa hisia huku akipiga gitaa mbele ya mashabiki wake waliofika kumshuhudia ndani ya ukumbi wa Diamond usiku huu.
Mashabiki kama kawa.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Linah na Amin wakiimbwa kwa pamoja wimbo mpya uitwa Mtima Wangu------------------------------------------------------------------------
Mshiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 kutoka Dar-Es-Salaam Walter Chilambo usiku wa kuamkia leo amekuwa mshindi wa jumla wa shindano hilo na kujinyakulia kitita cha shilingi za kitanzania Milioni 50 kama zawadi ya mshindi wa kwanza.

Walter aliibuka kidedea mbele ya Salma Yusuf kutoka Zanzibar ambaye walifaikiwa kuingia naye pamoja fainali ya washiriki wawili tu kati ya watano ambao walianza fainali hiyo hapo awali. Walter ambaye dalili za ushindi wake zilianza kuonekana tangu awali mwa fainali hiyo ameweka historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kujinyakulia kitita kikubwa katika mashindano ya kusaka vipaji vya muziki.

Aidha katika shindano hilo la kuamkia leo mshiriki Walter pamoja na wenzake walipitia hatua tatu ambapo ya kwanza ilikuwa kuimba na msanii mmoja mmoja waliowachagua ambapo yeye aliimba na msanii Ditto kabla ya kuimba mwenyewe katika raundi mbili zilizofiuata huku wakipigiwa kura na mashabiki katika raundi zote. 

Walter alitumia nyimbo moja ya Steve R n B “One Love”, na Nikikupata ya Ben Pol katika raundi zote mbili zilizofuata.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!