Saturday, December 1, 2012

"KIPAJI CHANGU KIPO NDANI YA BIFU".....SINTAH


MWANADADA mwenye makeke Bongo Christina John ‘Sinta’ amewaambia wapenzi wa filamu Swahiliwood kuwa yeye ni mkali wa filamu tangu kitambo lakini alikuwa ametingwa na mambo mengine ikiwa pamoja na masomo sasa karudi na uwezo wake kauonyesha katika filamu ya Bifu.


“Mimi ni mwigizaji mkongwe na mwenye uwezo katika hilo, nimerudi katika uigizaji kwa sasa nimeigiza filamu kadhaa lakini katika kuonyesha uwezo wangu angalia filamu ya Bifu nilivyowafunika wasanii nyota uwezo wangu upo juu katika kuigiza,”anasema Sinta.

Sinta ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi kiitwacho Harusini kinachorushwa katika televisheni ya Dtv anasema pamoja kuwa na kazi ya utangazaji bado si tatizo kwake kuweza kuigiza, huku akifikiria kuwa mtayarishaji wa filamu katika tasnia ya filamu.

Filamu ya Bifu inasambazwa na kampuni ya kizalendo ya Papazii Arts Entertainment & Promoters ya jijini Dar es Salaam, katika filamu ya Bifu imeshirikisha wasanii Farid Kubanda ‘Fid Q’, Mh. Joseph Mbilinyi ‘Mr. Sugu’, Christina John ‘Sinta’ na wasanii wengine nyota katika tasnia ya filamu.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!