Tuesday, December 25, 2012

EX GIRFRIEND WA NE-YO ALITAPIKA DAMU NA KUUGUA GHAFLA BAADA YA KUISIKILIZA INTERVEW YA NE-YO

Mkali wa RnB ambae pia ni mwandishi wa nyimbo Ne-Yo ametishiwa kuburuzwa mahakamani na girlfriend wake Jessica White baada ya mkali huyo kuendelea kuzungumzia kwenye interview mgogoro mkubwa kuhusu mtoto wao kwa sababu kwa kufanya hivyo anakuwa anaenda kinyume na makubaliano yao kuhusu mgogoro huo na kwamba anachozungumza kwenye interview zake kinamtesa sana Ex-girlfriend wake huyo.

Mwaka 2009, Ne-Yo na Jessica white walikubaliana kuwa Jessica alikuwa mja mzito na kwa maelezo yake na mahusiano yao wakati huo Ne-Yo aliamini kuwa ujauzito ni wa kwake..
 
 Ne-Yo alimpa mkwanja mama kijacho huyo kiasi cha $575, 000 kwa ajili ya maandalizi na mambo mengine. lakini baadae Jessica alimfafanulia Ne-Yo na kumueleza kuwa mtoto sio wa kwake, ni wa chalii mwingine, na hapo ndipo drama ilipoanzia.

Jessica White
Ne-Yo na Jessica walikubaliana kwamba wamalize tatizo lao bila kuliweka hadharani, kitu ambacho kinaonekana kumshinda Ne-Yo na anaonekana anazungumza mara kadhaa katika interview zake.

Mwanasheria wa Jessica White amemuandikia 'so sick hit maker' barua akimtishia kumfungulia mashtaka mahakamani kwa kosa la kuvunja mkataba wao, na kwamba kwa kufanya hivyo amemsababishia mateso makali Jessica White aliyesikiliza interview yake.

Jessica White alisema Ne-Yo alimzungumzia vibaya sana kwenye interview aliyofanya na kumfanya aonekane ni mtu mbaya sana kitu ambacho sio kweli. 
 
Na kwamba baada ya kusikiliza interview hiyo alijisikia kuwa amekashifiwa sana, na kunyanyaswa kitu kilichompelekea kuwa na ugonjwa usioleweka, akaanza kutapika, kutoka damu puani na nywele zake kunyonyoka.  
 
Alisema kutokana na hali hiyo alishindwa kwenda kazini na kulazimika kufungua file kwenye state aid, lakini pia akili yake haikuwa sawasawa wakati huo.

Haya sasa hii kweli ndo drama kali, akili imeunganisha mwili mzima na stress zikivuka mpaka ndo hivi unaweza kutundikiwa drip kadhaa za maji, Mapenzi bana..!


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!