Thursday, December 6, 2012

HATIMA YA MWINYI GOHA KURUDI MACHOZI BAND ITAJULIKANA NDNI YA "DIARY YA LADY JAYDEE"
Lady Jaydee
Baada ya Lady Jaydee juzi kuwaomba ushauri mashabiki wake kuhusiana na kama anatakiwa kumsamehe aliyekuwa muimbaji wa Machozi Band, Mwinyi Goha,mwanamuziki huyo mkongwe amesema hatma ya Mwinyi aliyejiondoa kwenye bendi yake itaoanekana kwenye reality TV show ya Diary ya Lady Jaydee.

Kupitia Facebook, Lady Jaydee ameandika, “Maoni ya wengi husaidia kubadilisha mawazo hata ya moyo uliokuwa mgumu kulainika, naheshimu mchango wa mawazo yenu kwani mmechukua muda wenu kuchangia swala la Mwinyigoha….

Kumsamehe tulishamsamehe mimi na uongozi mzima wa MACHOZI BAND .

Ndio maana hatukuwahi kuongelea chochote kilichotokea kwa upole au kwa jazba kwenye Media yoyote, ila swala la yeye kurudi au kutorudi kundini mtaliona ndani ya DIARY YA LADY JAYDEE, ambapo wanamuziki wenzake waliobaki Machozi Band baada ya yeye kuondoka wanaliongelea vipi??, na yeye mwenyewe amejielezea vipi? 

Usikose kuangalia DIARY YA LADY JAYDEE ndani ya EATV PEKEE, Uso kwa uso na mama mzazi wa Mwinyi, Captain G pamoja na JIDE. Sijakosea kuweka hii topic hapa, wanaoijua story toka mwanzo hawatanilaumu kwanini nime post.”
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!