Thursday, December 27, 2012

"RAY HAYAJUI MAUMBILE YANGU NA SINA UHUSIANO NAYE".....JOHARI


MSANII wa filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa, licha ya watu kudai kuwa yeye ana uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Vincent Kigosi ‘Ray’, anaapa hawajawahi kufikia hatua hiyo.

Akizungumza kwa kujiamini, Johari ameweka  wazi   madai hayo ni  ya uongo na anashangaa kuona watu wanazidi kukomalia.

“Naapa sijawahi kulala na Ray. Nashangaa hizi habari zinavyozidi kuenea. Kwa hilo niko tayari kushika hata Biblia kuapia kuwa sina na wala sijawahi kuwa na uhusiano na Ray, uhusiano wetu ni wa kikazi tu,” alisema Johari.


Johari kwa muda mrefu amekuwa akidaiwa kutoka na Ray kwa siri lakini mwenyewe anakana huku wadau wakizidi kushikilia kuwa habari hizo zina ukweli ndani yake.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!