Monday, December 17, 2012

HII NDO BURUDANI YA KOFFI OLOMIDE PALE LEADERS CLUB

Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries kupitia bia yake ya Tusker lager jumamosi jioni iliandaa tamasha maalumu kabisa la nyama choma pamoja na burudani ya muziki iliyopewa jina la Tusker Carnival na kumualika msanii nguli wa Kiafrika Koffi Olomide ambaye alikuja nchini maalumu katika tamasha hilo pamoja na kusherehekea kutimiza kwa miaka 13 kwa kituo cha Clouds Fm.


Tamasha hilo lilianza mapema mida ya alasiri ambapo wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar-es-Salaam na vitongoji vyake walikwenda katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kupata nyama choma huku wakishushia na bia yao pendwa ya Tusker Lager ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa tukio hilo.

Aidha katika kulipamba na kulinogesha tamasha hilo bendi kadhaa za nyumbani ikiwemo Twanga Pepeta, Mapacha watatu, Diamond Musica na Skylight Band zilialikwa kutumbuiza na kuwapa raha mashabiki na wapenzi wa burudani ya Muziki wa Dansi nchini Tanzania.

Bendi zote zilifanya makamuzi ya nguvu, lakini ushindani mkali ulionekana kutoka kwa bendi ya Diaomond Muzica iliyokuwa ikongozwa nae Hassan Liver Sultan na Bendi ya Skylight ambayo iliongozwa na kina Joniko Flower ambapo mashabiki wengi waliofika katika viwanja vya Leaders walionekana kuzifurahia.

Ilifika zamu ya msanii mwalikwa wa tamasha hilo la Tusker Carnival Charles Antoine Koffi Olomide ambapo alipanda stejini majira ya saa sita za usiku na ushehee akitanguliwa na mwimbaji wake mahiri wa kike katika kundi la Quartier Latin bibie Cindy ambaye naye alikonga nyoyo za mashabiki wengi waliojitokeza jana kwa sauti nyororo, murua na ya kuvutia.

Koffi Olomide alidumu kwa takriban saa moja akiimba nyimbo zake nyingi zaidi kutoka albamu yake ya nyuma Affaire D’Etat kama Julia na kadhalika. 


Koffi olomide alitumia wasaa wake wa kutumbuiza kuwashukuru watanzania kwa moyo wa upendo na ukarimu walionao kwake akisema amewapatia mashabiki wake wa Tanzania nafasi ndani ya moyo wake na pia aliwatambulisha washiriki wa kumsaka mrembo anayegombania taji la Miss East Africa jukwaani.

  Jumapili Koffi Olomide na kundi zima la quartier Latin wapo katika uwanja wa CCM Mwanza kutumbuiza kwa wakazi wa kanda ya ziwa.

waimbaji na wanenguaji wa kundi zima la Quartier Latin wakinengua.

CEO wa Clouds Media Joseph Kusaga akiteta na mkurugenzi mwenza Mama Juhaina Kusaga

Mwimbaji pekee wa kike wakundi la Quartier Latin Cindy akiwajibika pamoja na wacheza shoo.

Koffi Olomide akicheza na mmoja wa wagombea wa taji la urembo Miss East Africa wakati wa kuwatambulisha.

Koffi olomide akijiachia na Mmoja wa washiriki wa taji la Miss east Africa

Washiriki wa taji la Miss East Africa wakifuatilia shoo ya Koffi olomide kabla ya kutambulishwa jukwaani.

Wafanyakazi wa SBL Maurice Njowoka, Azda na Caroline wakipozi.

Babou wa kitaa na Rommie Jones wakiwakilisha.

Kitokololo wa Fm Academia akijiachia na Tusker yake.

Mwimbaji Cindy wa kundi la Quartier Latin akishambulia jukwaa.

Koffi olomide akijiandaa kupanda jukwaani.

Koffi Olomide akicheza Tcha choo style.

Koffi akimtambulisha CEO wa Clouds Media, Bwana Kusaga Jukwaani.

Koffi akiimba.

Warembo wa Miss East Africa.

Baraka Shelukindo wa Multi Choice TZ na mwenyekiti wa Taswa juma Pinto wakipozi mbele ya Camera


DSC_1868 (600x402)
DSC_1867 (600x402)
DSC_1866 (600x402)

Sam wa Skylight Banda na Shilole

Mtangazaji Musa Hussein na Khalid Chokoraa.Mtangazaji Musa Hussein na Khalid Chokoraa.

Warembo wa Miss East Africa wakipozi na Prisca Simon wa Fast Jet.

Mkurugenzi wa Serengeti Breweries bwana Steve Gannon akipozi na warembo wa Miss East Africa.

Wana Quartier Latin wakipozi backstage.


DSC_1811 (600x402)
DSC_1812 (600x402)
DSC_1817 (600x402)
DSC_1818 (600x402)

Msanii Dully sykes na Body Guard wake Arafat.

Fideline iranga alitokelezea na washkaji zake.

Shilole na swahiba wake.
DSC_1796 (600x402)

Sama pamoja na meneja wa Mapacha watatu na fan wao wakipozi kwa pamoja.

Mkurugenzi mtendaji wa SBL bwana Steve Gannon akicheza na Caroline.

Ben Kinyaiya akipozi na Mkurugenzi wa Masoko SBL Bwana Mafuru.
Mkurugenzi mtendaji wa SBL hakuwa na maskhara kabisa katika kuskata Rumba, hapa ilikuwa nyimbo ya Diaomond Musica.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!