Saturday, December 8, 2012

IRENE UWOYA AHAHA KUWAKIMBIA NDUGU WA ‘NDIKUMANA’ WALIOTUA DAR KUMCHUKUA MTOTO WAO


MSANII Irene Uwoya na mpenzi wake mcheza soka Ndikumana raia wa Rwanda baada ya kukaa kimya bila sekeseke lolote sasa hali imekuwa kubwa kwani inadaiwa kuwa ndugu wa mcheza soko huyo kutoka Rwanda wameigia nchini kumsaka Uwoya ili wamchukue mtoto wao kwa lengo la kumlea wenye.

Mwandishi wetu   alipewa ishu hiyo na mtu wa karibu sana na watu hao aliyefanikisha ndoa yao kufungwa, ambapo alidai kuwa kuna kundi la watu watano ambao ni ndugu wa mcheza soko huyo wameigia nchini kwa lengo la kumsaka Uwoya ili waondoke na mtoto wao.


Watu hao inadaiwa kuwa ni kaka mcheza soko huyo, dada, mjomba na wengine ni baadhi ya watu ambao walikuwa karibu katka ufanikishaji wa ndoa yao.


Jamaa huyo alidai kuwa watu hao wameigia dar kimya kimya na wamefikia kwenye hotel moja iliyopo Kariakoo, lakini inaonesha wazi ujio wao si bure kuna kitu kikubwa wamekuja kufanya, ambacho kinamuhusu Uwoya na mtoto wake.


Chanzo chetu kilidai kuwa ndugu hao wa jamaa wamekuja tangu wiki iliyopita na kuna dada mkubwa wa Ndikumana ambaye anaongoza msafara huu ambaye alikuwa ni mtu wa karibu na Uwoya katika harusi yao.


“Ndugu wa Ndikumana wametua nchini kutaka kumchukua mtoto wao na inawezekana ishu hii itakuwa imefanya na jamaa baada ya kuona mapenzi yameisha, ujio wao umemshtua sana Uwoya kwani sasa ana haha kutafuta sululu lakini bado hajapata jibu,” kilisema chanzo hicho.

Wakati huo huo mtandao huo ulipomtafuta Uwoya ili kueleza juu ya ishu hii alipopigiwa simu mara kadhaa iliita bila mafanikio ya kupokelewa na dakika ya mwisho alipopigiwa alipokea lakini hakuweza kuzungumza chochote kwa madai yuko bize na mtoto kwani alisikika akilia sana.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!