Friday, December 14, 2012

KOFFI OLOMIDE AWASILI JIJINI DAR AYARI KWA SHOO SIKU YA JUMAMOSIMwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki  usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba.....


Onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey KusagaMkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza na (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar  usiku wa kuamkia leo

 Baadhi ya wanamuziki wa Koffi Olomide wakishuka kwenye gari kwenye viunga vya hoteli ya Serena usiku wa kuamkia leo .

 Baadhi ya wadau na wapenzi waliokumbana uso uso kwa na mwanamuziki Koffi Olomide usiku wa kuamkia leo,wakipata picha ya pamoja.

 Mdau Idd Janguo nae alipata picha ya ukumbusho na Koffi Olomide,ambaye anasema amejipanga vyema kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar siku ya jumamosi ndani ya vuwanja vya Lidaz Club.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!