Tuesday, December 18, 2012

KUBAKWA KWA SHILOLE BADO NI CHANGAMOTO KUBWA MAISHANI MWAKE HASA SIKU KAMA YA LEO AMBAYO NI "BIRTHDAY YAKE"


Msanii wa Bongo Movie na Bongofleva Shilole aka mtoto mzuri leo anasherehekea siku yake kuzaliwa.Ikiwa leo ni siku yake muhimu kwake si vibaya ukafahamu baadhi ya vitu kuhusu yeye. 


Miongoni mwa mambo mengi, jambo ambalo bado  nimtihani  mgumu kuusahauni lile  sakata  la kubakwa....yafuatayo ni  baadhi ya mambo  yanayomhusu  shilole.

1.Shilole ametimiza miaka 25 hii inamaana alizaliwa tarehe 18 mwezi 12 mwaka 1987.


2.Shilole ana watoto wawili alipata mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka 16


3.Mpaka sasa Shilole ashacheza movie/filamu 17

4.Shilole ana nyimbo 4, ngoma ya kwanza 'Lawama', ya pili 'Dume Dada', ya tatu 'Viuno' na ya nne ni 'Dudu'


5.Shilole anasema kuwa msanii aliyemvutia yeye kuimba ni Ray C


6.Shilole anamiliki maduka mawili ya nguo na pia na mpango wa kufungua Cafe hivi karibuni


7.Shilole alishawahi kubakwa akiwa mdogo na ndo hapo alipopata mimba nakumlazimu kuacha Shule.


8.Shilole alizaliwa Tabora nakukulia huko baadae ndo akaja Dar es salaam


9.Shilole hivi sasa analipwa shilingi milioni 2 kwenye shoo


10.Rangi anayoipenda ni Pink.

HAPPY B'DAY SHILOLE.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!