Saturday, December 1, 2012

"NINASTAHILI KUPEWA TUZO" – MONALISA.

NYOTA wa filamu katika tasnia ya filamu Swahiliwood Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ anaamini kuwa anastahili kuendelea kuwa ndiye mwigizaji bora wa kike katika tasnia ya filamu Tanzania, huku akiamini si kitu kinachopatikana kirahisi bali ni juhudi zake na kuwa makini kwa kile anachokifanya katika tasnia ya filamu.


“Nawashukru waandaaji wa tuzo mbalimbali japo kuwa taasisi husika zimekuwa zikizuia utoaji wa tuzo kwa wasanii wa filamu bila sababu za msingi na kila zinapotolewa kihalali lazima nang’ara kwa sababu mimi ni bora na ninastahili kupata tuzo,”anasema Monalisa.

Monalisa ni moja kati ya wasanii waasisi wa tasnia ya filamu hivi karibuni alitangazwa kama mwigizaji bora wa kike mwaka 2012 huku tuzo ya mwigizaji bora wa kiume ikienda kwa marehemu Steven Kanumba tuzo hizo zilitolewa na Jarida la Bab kubwa, Monalisa ameshinda nyingi kama Tuzo za BORA ZA 2010, tuzo za ZIFF.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!