Saturday, December 29, 2012

"NAWAPENDA MARAFIKI WA KIUME MAANA HAWANA MAJUNGU KAMA WANAWAKE".....QUEEN DARLEEN


STAA anayefanya poa na ngoma ‘Kokoro’, Queen Darleen, ameuambia mtandao huu  kuwa anajisikia raha kuwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wanawake, huku akiamini kuwa tabia za baadhi ya wanawake ndizo zinazomfanya awe hivyo.

Msanii huyo ni mmoja ya wanawake wenye staili za kipekee kabisa kwenye game ingawa ndani ya mwaka huu amekuja kivingine kabisa baada ya kuwa kimya kwa muda na kuteka mashabiki kupitia kibao cha ‘Maneno Maneno’.


Kauli ya msanii huyo imekuja baada ya kuzungumza na mwandishi wetu alietaka kujua ni kundi gani la watu ambao hupenda kuwa nao karibu sana na kubandilishana mawazo ndipo yenye maana, ndipo alipofunguka kuwa mara nyingi huwa karibu na wanaume na si wanawake.


Alisema kuwa karibu na wanaume haimanishi kwamba ni mabwana zake hapana bali anaona ni watu ambao anaendana nao ingawa tabia zake si za kiume kama baadhi ya watu wanavyopenda kudhani kutoka na staili zake au aina ya kazi anazofanya.


“Kuna watu wanajua mimi nina tabia za kiume hiyo inawezekana kwa sababu wao ndo wanaosema, napenda sana kuwa na watu ambao tutafanya mambo ya maendeleo na si kuzungumza mapenzi na upuuzi muda wote hiyo ndo sababu kubwa inayonifanya nijiweke sana kwa wanaume,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa anahisi akijiweka karibu sana na wanawake hakuna kitu kikubwa watakachokuwa wanazungumza zaidi ya majungu na mapenzi, ingawa hata wanaume baadhi yao wako hivyo ila si kama wanawake ambao hupoteza mda mwingi kujadili ujinga.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!