Thursday, December 20, 2012

MR.CHUZ WA "JUMBA LA DHAHABU" AJIPANGA KUJA NA TAMTHILIA NYINGINE MWAKANI IITWAYO " HIGH HEELS"Muongozaji na muigizaji wa filamu nchini Tuesday Kihangala aka Mr Chuzi anatarajia kuja na tamthilia mpya ya TV iliyopewa jina ‘High Heels’.


Tamthilia hiyo itakuwa na waigizaji wengi wa Jumba la Dhahabu ambao ni pamoja na Jini Kabula,Rayuu, Kojack,Bi Moza, Kilomani,Badi,Kishoka na wote waliokuwepo kwenye Jumba la Dhahabu.Pia kutakuwepo na wasanii wengi wachanga.

Akiongea kwa kujiamini, Rayuu ambaye ataigiza kwenye tamthilia hiyo amesema High Heels itakuwa zaidi ya Jumba la Dhahabu.

“Wajipange wauza sura, ni funiko babkubwa kwani kila mtu kapania kuonyesha uwezo wake,” amesema Rayuu.
Rayuu
“Humo utakutana na utapeli, uchawi, ujambazi, mapenzi ,visasi nk. Sasa katiki hii  ndo utaelewa kwanini imeitwa viatu virefu na pia kwa Tanzania itaanza kutoka kwenye DVD ndo itarushwa kwenye TV.”

Rayuu amesema tamthilia hiyo itaanza kuonekana nchini mwezi January mwakani pamoja na nje ya nchi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!