Wednesday, December 19, 2012

"SIKUMBAKA NANCY BALI ALINIKUBALI MWENYEWE"......MAPUNDA WA STEPS ENTERTAINMENT


SIKU chache baada ya kuibuka kwa skendo ya ubakaji inayomkabili prodyuza maarufu wa filamu Bongo ambaye pia ni Msemaji wa Kampuni ya Steps Entertainment, Seles Mapunda ameibuka na kufungukia ishu hiyo.

Akizungumzia ishu hiyo  hivi karibuni Mapunda kwanza alisema kuwa hakumbaka Nancy Njozy aliyefungua kesi katika kituo cha polisi cha Oysterbay bali msichana huyo anatafuta umaarufu ambao amekuwa akiusaka kwa muda mrefu.

“Sikumbaka Nancy na wala haiwezi kuwa hivyo, nadhani anatafuta umaarufu.


 Hiyo siku ya tukio anayoizungumzia, yeye mwenyewe ndiye aliyenitafuta akitaka tukutane nimpe penzi, kutokana na kunilazimisha sana nilikubaliana naye, tukaenda kwenye ‘lodge’ moja, iko pale Mwananyamala.

“Tukiwa hapo tukipeana raha, mara mlango ukagongwa na meneja wa ‘lodge’ hiyo na kuniambia kuwa, kuna watu walikuja kugonga getini wakidai mimi nimeingia na mke wa mtu pale.


“Nilishangaa kusikia kuwa Nancy ni mke wa mtu, nilipomuuliza kuhusiana na watu hao akaanza kulia na kuniambia kweli ana mtu wake ambaye alishamtolea mahari, hapo ndipo nikabaini kuwa nimefanyiwa mchezo. Nikavaa nguo zangu na kuondoka,” alisema Seles na kuongeza:

“Baada ya dakika 20 nikiwa Ambiance Bar, Sinza ikaingia sms kwenye simu yangu toka namba 07146786… imeandikwa hivi; ‘we (tusi) unajifanya msanii sio? Unatembea na demu wangu, nita(tusi), unaujua msitu wa Mabwepande? Kama huujui kamuulize Dokta Uli, nitakufanyizia utakoma’. 


Sikujibu kitu, asubuhi nikaendelea na shughuli zangu kama kawaida hadi nilipokuja kuambiwa kuwa nimefunguliwa kesi ya ubakaji na demu huyo.”

Kesi hiyo ya ipo katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar kwa faili lenye kumbukumbu namba OB/RB/20861/2012 UBAKAJI.


SOURCE:  GPL
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!