Saturday, December 8, 2012

PROFESA JAY ASHAURIWA KUANZISHA WEBSITE YAKEDully Sykes, Diamond, Cpwaa, AY, Mwana FA, Tunda Man, Ditto, Lady Jaydee, Solothang kutaja wasanii wachache tu, tayari wana website/blog zao. Japo sio zote zinazokuwa active kila siku lakini yatosha kwa mashabiki wao kupata machache kutoka kwao.


Lakini kuna msanii mmoja mkubwa nchini Tanzania ambaye ana kila sababu ya kujiunga na wenzake hao tuliowataja kwa kuwa na website yake mwenyewe. Si mwingine ni Joseph Haule aka Profesa Jay. 

Kutokana na umuhimu mkubwa wa Profesa kwenye muziki nchini, msomi na mwandishi mahiri wa makala aliyepo masomoni nchini Scotland, Evarist Chahali amemshauri mchawi huyo wa rhymes kuanzisha website yake.

“Halafu Prof, kuna umuhimu kwa heavyweight emcee kama wewe kuungana nasi kwenye masuala ya kublogu…au kuwa na tovuti kamili,” ametweet Chahali.

Ushauri huo umepokelewa vema na Profesa Jay aliyejibu, “ Hilo la kuhusu blogu umeongea jambo la msingi sana mkuu nitalifanyia kazi kwa umakini sana kisha nitakwambia inakuwaje kiongozi.”

Kwakuwa tunafahamu jinsi Joseph anavyopenda soka, website yake huenda ikageuka kuwa chanzo kimoja kizuri cha habari za michezo ama sio?


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!