Friday, December 14, 2012

SHILOLE AKIDENDEKA NA MWANAMKE MWENZIE....


MSANII wa filamu ambaye pia anafanya muziki, Zuena Mohammed ‘Shilole’  na demu mwenzake aliyefahamika kwa jina la Hawa Juma ‘Mama Ayana’ hivi karibuni waliwaacha watu midomo wazi baada ya kugandana kimahaba mbele za watu. 

Tukio hilo lilitokea Msasani jijini Dar kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi ambako kulikuwa na pati ya kusherehekea kuzaliwa kwa Hawa.

Wakiwa eneo hilo, wawili hao walionekana kuwa karibu sana na lilipofika zoezi la kulishana keki na kufika zamu ya Shilole aliyekuwa MC, Hawa aliweka pembeni ‘stiki’ aliyokuwa akiitumia kulishia watu wengine kisha kutumia mdomo wake kumlisha msanii huyo.


Kitendo cha wawili hao kugandishiana midomo yao huku wakionekana wenye hisia, kilichukua muda wa takriban sekunde 60, mazingira yaliyowafanya baadhi ya waalikwa kuanza kunong’ona kuwa, kilichofanyika ni usagaji.


==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!