Thursday, December 6, 2012

"ADUI SIO MTU WA KUMSAHAU HATA KAMA HUNA KINYONGO NAYE"...LORD EYEZ

Kwenye exclusive interview na Clouds fm, rapper kutoka A City Lord Eyes amefungua mengine kutoka moyoni mwake kuhusu fitna zinazofanywa dhidi yake.

 ” Hata mambo yanavyoenda nafikiri wewe mwenyewe unaona na kuna vitu pia nimeviona na kuna watu pia nimewaona, unajua adui sio mtu wa kumsahau hata kama hauna kinyongo nae lakini usimsahau kwamba ni adui”LORD EYEZ

Baada ya kuyasema hayo Lord Eyes ambae yuko nje kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi kwa zaidi ya siku 10 kutokana na tuhuma za wizi wa vifaa vya gari la msanii Ommy Dimpoz hakutaka kuendelea tena kuzungumza ila hiyo ndio msg fupi aliyotaka kuizungumza.

Mpaka sasa amesema ni nyimbo tatu alizonazo kichwani zenye mistari kuhusu kilichomkuta kwenye tuhuma hizo za wizi ambazo atazitoa na kuna uwezekano moja akaitoa december hii.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!