Saturday, December 22, 2012

TATU BORA YA WAIGIZAJI WA KIUME WA BONGO MOVIE- 2012

Mtandao huu ukishirikiana na vyanzo  mbali mbali vya habari  umefanya  tafiti na kubaini majina  matatu ya  wasanii nguli  katika tasnia  ya maigizo  hapa nchini.....


1. Jacob Stephen

Mwigizaji Jacob Stephen amekuwa na mafanikio makubwa katika kazi zake ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki baada ya kubeba uhusika kama inavyo takiwa na kufanya mashabiki wake kuvutiwa na kila kazi anayoitoa.


JB mwenye umri wa miaka 52 kwa sasa ana miliki kampuni yake ya Jerusalem Film Company ambayo inafanya vizuri baada ya kuzalisha filamu zaidi ya 23.
2. Vincent Kigosi 

Ray The Greatest amekubalika na jamii kwa ubora wa filamu zake za mwaka jana ikiwemo Sister Marry.

Yeye na Brandina Chagula a.k.a Johari waliamua kujiunga na kuanzisha kampuni ya kuzalisha filamu iitwayo RJ Company.3. Hisany Muya "Tino"

Katika soko la filamu Tino ni actor anayekuja kwa kasi kwenye filamu za mapigano ama action. Mwaka huu ametisha na filamu yake iitwayo CID.


Hapo awali Tino alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu nia yake ya kuachana na kuigiza filamu za mapenzi na kuamua kufanya za action ambazo ameonesha kuziweza.

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!