Thursday, December 6, 2012

UGONJWA WA MOYO WAMTESA SNURA


HALI ya msanii kiwango wa filamu za Kibongo, Snura Mushi ‘Snura’ siyo nzuri kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa Moyo.

Akizungumza na paparazi wetu aliyemtembelea msanii huyo hivi karibuni nyumbani kwake, Mwananyamala, Dar es Salaam baada ya kupata taarifa ya kuumwa kwake, msanii huyo alisema anaumwa sana.


Msanii huyo alisema kuwa, kadiri siku zinavyokwenda ndivyo maradhi hayo yanazidi kumshambulia.

Aliongeza kwamba, tatizo hilo lilimuanza alipokwenda  Muheza, Tanga kuhudhuria msiba wa Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo Milionea’.

“Yaani sina hamu ya kula, kutapika ndiyo huku, sijui ni hizi dawa za malaria nilizomeza ndiyo zinasababisha hali hii,  naumwa sana jamani...niombeeni kwa Mungu nipone,” alisema Snura.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!