Tuesday, December 18, 2012

UGUMU WA MAISHA WAPELEKEA KIJANA KUJIFANYA MCHUNGAJI


 Kijana ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja kutokana na hali aliyoionyesha akiwa anaongea kwa lugha ambayo haieleweki na huku akilia kwa sauti hadi kupelekea watu kujazana na kutaka kujua anachofanya mbele ya gari hilo huku biblia ikionekana kwa karibu.
 Hapa sasa Chanzo cha Yeye Kulia na Kunena kwa lugha kama walokole wanavyofanya kikajulikana huku alipodai kuwa kwenye gari hilo kuna majini ndio maana ameamua kuliombea ili watoke.
 Mchungaji Jina akilia kama huku akiwa anatoa maneno yasiyoeleweka kwa kujifanya yeye ni mchungaji na hapo akiombea gari hilo analodai kuwa lina mapepo
Baadhi ya wakazi wa eneo la Mtaa wa Msimbazi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumshangaa kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja baada ya kujifanya mchungaji huku akidai kuwa gari hilo mbele yake lina mapepo na ndio maana ameamua kuliombea hili yaweze kutoka. hayo yote yametokea jana jioni  kwenye Mtaa wa Msimbazi karibu na Kituo cha Daladala cha Mbezi.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!