Wednesday, December 19, 2012

UNYAMA: VIDEO YA KIJANA MMOJA ALYECHOMWA MOTO KWA KOSA LA WIZI......


Hakika  kuna jamii zenye  roho za simba......!!!

Kijana mmoja  amejikuta  mikononi  mwa wananchi wenye hasira kali  baada ya kutuhumiwa kuiba......

Wananchi hao  walitoa kichapo kikali  kwa  kijana huyu , hali iliyomfanya  ajeruhiwe vibaya.....

Kama vile haitoshi, wananchi hao walifikia  maamuzi mabaya  baada  ya  kuamua  kuyakatisha maisha ya kijana  huyu kwa kumchoma moto....!!!

Ni  kweli wizi ni mbaya ,  lakini iko  haja  sheria  zikaachwa  zichukue  mkondo  wake  kuliko  kujichukulia maamuzi mabaya  kama haya.......

Tukio  hili limetokea nchini  Nigeria, lakini ni vema likawa fundisho  kwetu  juu  ya  ukatili na unyama huu maana ni jambo ambalo halikubaliki katika nchi yoyote

 
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!