Friday, December 7, 2012

UPDATE: JOHN MNYIKA ASHINDA RUFAA YA KUPINGA USHINDI WAKE KATIKA JIMBO LA UBUNGO


Mbunge wa jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, John Mnyika, ameshinda rufaa ya kupinga ushindi wake wa Ubunge katika jimbo hilo.

Hiyo ni baada ya aliyekuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 Hawa Nghumbi(CCM) aliyekata rufaa dhidi ya matokeo ya ushindi wa Mnyika kuondoa rufaa yake asubuhi ya leo.

Kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufani.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!