Friday, December 21, 2012

VIDEO INAYOMUONESHA MSANII WA FILAMU BONGO ( SHAMSA FORD) AKIJIFUNGUA YAVUJA NA KUSAMBAA....VIDEO inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford akijifungua imezua kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana kuichukua bila ridhaa ya mhusika na kuisambaza kwa watu mbalimbali.
 

Akizungumzia  suala hilo  hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Shamsa alisema kuwa, video hiyo msanii huyo alirekodiwa kwa ajili ya kumbukumbu zake lakini ameshangaa kusikia kuna baadhi ya watu wanayo.

“Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa anahaha kumjua aliyeisambaza lakini pia anahakikisha haiwafikiii watu wengine na vyombo vya habari kwani inamuonesha hatua kwa hatua akijifungua,” kilisema chanzo hicho


Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Shamsa ambaye alisema: “Kiukweli nimeumia sana, hiyo video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu, kwa nini mtu aichukue na kuisambaza bila ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”

 ----------------
Mtandao huu  haujafanikiwa  kuipata   video hiyo...
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!