Friday, January 4, 2013

AMINI NA LINEX WAUNGANA TENA NDANI YA "USIKU WA MTIMA WANGU"Baada ya kufanya show kali katika fainali za BSS mwishoni mwa mwaka jana na kuzua mjadala kama wapenzi hawa wa zamani wamerudiana, wasanii wa THT Amini na Linah wanatarajia kufanya show nyingine pamoja huko Kigamboni, Dar es Salaam waliyoipa jina la ‘Usiku wa Mtima Wangu’.


Show hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Club Kakala siku ya Jumamosi ya January 5 ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 6,000 tu.

Wasanii hao kwa sasa wana wimbo mpya uitwao Mtima Wangu unaofanya vizuri kwenye vituo vya radio.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!