Monday, January 7, 2013

BAADA YA "NATAKA KULEWA"....DIAMOND SASA AANZA KUPIKA NGOMA MPYA NDANI YA AM RECORDSUmepita muda mrefu tangu kuzuka kwa ile scandal kubwa iliyomwandama Diamond na producer wake Manecky ya kudaiwa kuiga idea ya nyimbo za H Baba na Pasha. 

Licha ya kuamua kufanya video ya wimbo huo ulioleta maneno mengi, Nataka Kulewa, Diamond aliamua kuupotezea na kuachia ngoma nyingine iliyotengenezwa na Marco Chali, ‘Kesho’ ambayo video yake iliyofanyika nchini Kenya chini ya Ogopa Djs ikiwa miongoni mwa video kali kabisa zilizotoka hivi karibuni.


Na sasa Diamond na Manecky wamekutana tena kufanya kile wakifanyacho kwa ubora. Kupitia website yake, Diamond ameweka picha akiwa AM Records na Manecky na kuandika:
manecky 2

"Leo tangia nimeamka nilikuwa na Mzuka wa kufanya ngoma…Nikaona sio kesi ngoja nimvutie waya Maneck…

Eeeeh! nasasa hali iko hivi hapa Am Rec. Ni moja ya wimbo wa tofauti sanaaaa.."
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!