Friday, January 18, 2013

BRITISH AIRWAYS YASITISHA SAFARI ZA DA ES SALAAMBaada ya miongo minne ya kutoa huduma nchini Tanzania, hatimaye shirika la ndege la British Airways limeamua kusitisha safari zake za kuja nchini kwa madai kuwa ilikuwa ikipata hasara.


Maelezo kutoka kwa shirika hilo yalisema, “”Dar es Salaam was not performing well from a commercial perspective so we have taken the decision to suspend the route.”

Kwa mujibu wa maelezo hayo, abiria waliokuwa wamebook kusafiri kabla ya March 31 watarudishiwa fedha zao ama kuhamishiwa kwenye ndege zinazoishia Nairobi, Entebbe ama Lusaka.

Uamuzi huo unadaiwa kuwa utaathiri uchumi wa Tanzania kwa namna nyingi ikiwa pamoja na kupungua kwa watalii kutoka nchini Uingereza na mambo mengine
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!