Monday, January 7, 2013

CHADEMA WAAMUA KUIGAWA NCHI KATIKA MAJIMBO 10Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika mapendekezo ya chama chake (CHADEMA) kuhusiana na tawala za majimbo na serikali za mitaa ambayo ni miongoni mwa mapendekezo yao katika katiba mpya.


1. Nchi ya Tanganyika itagawanywa katika maeneo kumi ya kikanda yatakayojulikana kama Majimbo kama ifuatavyo:

(a) Jimbo la Nyanza Magharibi ambalo litaundwa na mikoa ya sasa ya Kagera, Geita na Shinyanga;
(b) Jimbo la Nyanza Mashariki litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Mara, Mwanza na Simiyu;
(c) Jimbo la Ziwa Tanganyika litakalojumuisha mikoa ya sasa ya Kigoma, Katavi na Rukwa;
(d) Jimbo la Kati litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Tabora, Singida, Dodoma na Iringa;
(e) Jimbo la Kaskazini litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara;
(f) Jimbo la Pwani ya Kaskazini litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Tanga, Wilaya za Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kisarawe na Mkuranga katika Mkoa wa sasa wa Pwani na Wilaya za Gairo, Kilosa, Mvomero, Morogoro na Kilombero katika Mkoa wa sasa wa Morogoro;
(g) Jimbo la Mji Mkuu wa Dar es Salaam;
(h) Jimbo la Pwani ya Kusini litakaloundwa na mikoa ya sasa Lindi, Mtwara na Wilaya za Rufiji na Mafia katika Mkoa wa sasa wa Pwani, na Wilaya ya Ulanga katika Mkoa wa sasa wa Morogoro;
(i) Jimbo la Nyanda za Juu Kusini litakaloundwa na mikoa ya sasa ya Mbeya, Njombe na Ruvuma;
2. Majimbo yataongozwa na Gavana atakayechaguliwa moja kwa moja na wananchi katika Jimbo husika.
3. Miji, manispaa na jiji ndani ya majimbo itaongozwa na Meya atakayechaguliwa moja kwa moja na Wananchi katika Mji husika;

Hata hivyo mapendekezo hayo yamepokelewa kwa hisia tofauti kama ifuatavyo:

Kaiche Milanzi
Hiyo ni kwa mujibu wa sera zenu chadema mlivoelekezwa na wazungu wenu wanaowapa misaada au?

Kiyao Chibas Kush
Mkoa wa Iringa hauwezi kua jimbo la kati mkoa wa Iringa ni nyanda za juu kusini ambapo ukanda huu ukiwezeshwa ndio utalisha nchi…..haiwezekani Iringa kua jimbo la kati muheshimiwa

Njiku Frank
Safi sana mkuu kwa kuja na hii taarifa,rai yangu kwa kwako(CHADEMA) inatakiwa mtoe Elimu zaidi kwa JAMII kuhusu Utawala huu wa MAJIMBO,MAANA yake,FAIDA zake ,CHANGAMOTO ZAKE zinaweza kujikotokea na jinsi gani mtakavyozikabili,nchi zipi duniani zinazofuata mfumo huu,hali zao kimaendeleo kwa sasa zikoje,na hapa ndipo ninapoomba tena na tena CHADEMA IANZISHE TV na RADIO yake haraka..nawasilisha

Simba Zubery

Yaan hcho ndicho mnapeleka mbele ya jaji mstafuu na huku mkienda na mwanasheria Tund lissu na m2 makin kama ww kuwa mbele kwa kupeleka maneno ya Tanganyika na matabaka..naomba ujipange broo labda umpe mnyka apeleke na msimtumie Tundu lissu hata page mmoja..


Ben Mwanantala
Kwani haya mapendekezo mmeyajadili kwa masaa mangapi,,,,,zitto,,,maana kwa hizi comments inaonesha kuna sehemu mmeenda wrong…Hebu fikirieni upya maana nyie ndiyo chama kikubwa cha upinzani mkiteleza tuu…CHADEMA MTAKUWA MMEIPOTEZA TALANTA,,,nawasihi sana

Sam Van der Lang
Umechunguza na kujua mazara ya majimbo au umeamua tu???hayo ni matabaka, jaribu kufanya study…mikoa kama lindi na mtwara unazan itaendelea vip na more than 70%ni pori na hamna wakuendeleza????kwa hilo mutachemka…afu futa utanganyika hapo…wapi visiwa vya unguja na pemba????jipange mzee…tunawapenda coz tunataka mabadiliko ila munavulunda sana…

Apollo Temu
Inasikitisha kung’ang’ania majina na mipaka ya Kikoloni ya Berlin 1885 – kumbe kweli akili zetu hawa wakubwa walizikamata kwa vizazi hadi vizazi! Tupeleke madaraka makubwa wilayani sio kuweka tabaka nyingine za uongozi. Tutunze na Kulinda Muungano. 

Mataifa makubwa yako busy kuungana sisi vijinchi vidogo vidogo leo 21st century tuko inward looking! This is a GRAVE mistake! Viongozi wetu haya kama hamyaoni basi sikilizeni maoni yenye umbali sio short term popularity. Tusiende kwenye cheap politics at such massive cost. 

Tena hizo powerful nations kimya kimya watakuwa wanasema gawanyikeni na kutoa sababu za kufeli kwao kwenye similar projects ila hawakuambii kwanini they still stay the cause of unity and will never drop. Ila wewe vunja vunja nchi. Na anajua unajua sio busara yet you go ahead with it ! Hapana, tujiangalie upya kwa hili !

Peter Piere Amandus
Haha! Zitto>huu mfumo mnaousema, kwanza hyo Tanganyka haipo.. Ni mfumo mzuri, lakn je, hyo tanganyka iko wapi? Kuhusu utabaka, mimi cdhan kama kutakuwa na utabaka,mana kama ni utabaka ungekuwepo kwenye mikoa, mfumo huu hauna tofaut xana na mfumo wa mikoa ya kawaida, tofaut kuu ni kuwa mfumo huu umekusanya maeneo meng na kuwa 1, ila mmekosea kuendelea kuufanya mji wa dar ujitegemee… 

Kama ni suala la muungano, jbu la kero za muungano ni aidha 1. Kuwa na serikali moja au 2. Kuvunja muungano, bs! Likshafanyka hlo 2tasonga mbele, ila mnavyotaka kuirejsha tanganyka mkumbuke mnaongeza serikali ya 3, hyo ni mzgo kwa sisi wananch walipa kodi.. Ni hayo 2
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!