Tuesday, January 8, 2013

CHAMELEONI NDANI YA MTEGO MZITO.....YAWEZEKANA AKASHITAKIWA KWA KOSA LA MAUAJIMwanamuziki wa Uganda , Jose Chameleone anaweza kujikuta akikabiliwa na kesi ya mauaji kutokana na kifo cha kijana mwenye miaka 27, Robert Karamagi aliyefariki hospitali baada ya kujichoma moto nyumbani kwa mwanamuziki huyo.


Joseph Mayanja na mke wake Daniella Atim Mayanja na wengine wanaoishi nyumbani kwake wanafikiriwa na polisi kuhusu kushtakiwa kwa kifo Karamagi.

Ripoti za awali zinadai kuwa Karamagi alijaribu kupora nyumbani kwa Chameleone lakini alikuwa na nia ya kumuua Daniella. Hata hivyo kwa bahati mbaya alijichoma moto mwenyewe uliomsababishia majeraha na hatimaye kifo.
Daniela (mke wa Chameleone)Daniela (mke wa Chameleone)
Baba yake amezikataa taarifa kuwa mwanae alijichoma moto na kudai kuwa alimpigia akiwa hospitali kumwambia kuwa Chameleone na washkaji zake walimpiga, kumtesa na kumchoma moto.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!