Friday, January 4, 2013

DIAMOND AFUNGUKA KUHUSU FUJO ZILIZOTOKEA WAKATI WA SHOW YAKE PAMOJA NA HASARA ILIYOPATIKANA


Usiku wa january 1 2013 Maisha Club ulikua usiku maalum kwa show ya WASAFI ambao wanaongozwa na Diamond Platnums, usiku huu umeingia kwenye Headlines baada ya fujo kubwa kutokea za kurushwa chupa, viti na mayai viza.
Noma ilianza dakika 15 baada ya Diamond kuanza kuingia kwenye stage ambapo anakiri kwamba alijua kulikua kuna watu wamepanga kuja kumfanyia fujo na aliuambia uongozi wa Maisha Club mapema kwa tahadhari na wakamwambia aendelee manake wameshaongea na wahusika lakini kumbe maongezi hayakubadilisha chochote.
Anavyosema Diamond ni kwamba waliofanya fujo ni washkaji zake wa siku nyingi ambao alikua nae Kariakoo, hao washkaji walikua wamegombana hivyo kugawanyika katika makundi mawili ambapo kundi moja lilikua linataka Diamond awe nalo alafu jingine alitenge, anasema yeye alikataa hilo wazo kwa sababu wote ni washkaji zake.
Huo msimamo ulifanya hilo kundi lililomshawishi kukasirika na kuamua kulipiza kisasi kwa kufanya fujo Maisha Club, taarifa alizipata mapema kwamba wangekuja kumzomea ambapo kweli hao jamaa walipofika Maisha wakati wa show walianza kuzomea lakini Diamond akatangaza kwa mashabiki ambao walimsupport Diamond na kupiga kelele zilizowashinda hao wazomeaji ambao baada ya kuona hivyo walianza kufanya fujo.
 
Mmoja wa hao wazomeaji ambae aliongea na millardayo usiku huo huo kwenye eneo la tukio alisema wao hawahusiki na fujo zilizotokea, waliofanya fujo ni mashabiki tu ambao pengine walichoshwa na show ya Diamond, wao walichokuja kufanya ilikua ni kuzomea tu kwa sababu Diamond alikiuka makubaliano yao.
Makubaliano yenyewe ni kwamba kwa sababu Diamond ni mshkaji wao toka kitambo kabla hajajulikana kisanii, walishakubaliana toka wakati huo kwamba akifanikiwa kimuziki inabidi asaidie na washkaji wengine wa kundi hilo ambao ni wasanii wachanga kitu ambacho jamaa wanadai Diamond hajakifanya kabisa, siku ya tukio alitakiwa kuperform na msanii mmoja wapo aitwae Papaa Masai lakini Diamond alikataa na hicho ndicho kilichowapa hasira.
Baada ya mambo kuharibika hili kundi pia limedai kwamba kuna wakati Diamond alikua anawatuma kwenda kumzomea Bob Juniour kwenye show zake na pia alikua anawatumia kwenye show zake kwenda kumshangilia.
 Diamond amesema wote waliomfanyia fujo anawajua mpaka kwa majina na tayari ameshawashitaki polisi na atahakikisha wakienda kukamatwa wanakamatwa kukiwa kuna kamera inawarekodi ili waonekane.
Kitu kingine alichokisema ni kwamba kati ya hao waliokwenda kumfanyia fujo ni pamoja na mdogo wa msanii ambae aliwahi kuwa na ugomvi nae wakapatana (huyo msanii) lakini bado huyo msanii amekua na chuki dhidi yake.
Yani Diamond aliwahi kuwa na beef na huyo msanii wakayamaliza lakini bado jamaa ana chuki, hawezi kumtaja kwa sasa na anachofanya ni kuacha uchunguzi wa polisi ufanyike kwanza, ikigundulika ni kweli atamtaja hadharani.
Kuhusu huyo msanii namkariri zaidi Diamond akisema “Uhusiano wangu na huyu msanii hauko vizuri, tulishahitilafiana kama mwaka umepita tukapatana lakini bado ana chuki dhidi yangu, tatizo niliona liliisha lakini nikaona mwenzangu kama bado ananionyesha chuki hata nikikutana nae najifanya kama hakuna tatizo lakini moyoni najua mwenzangu kuna vitu ana viendeleza vya chinichini ambavyo sivielewi”
Diamond amesema hasara ya vitu vyake kwenye hizo fujo ina thamani ya milioni zaidi ya 13 kutokana na kuibiwa simu yake ya iPhone5, cheni pamoja na camera ya video ya thamani kubwa ambayo aliinunua kwa ajili ya website yake.
CREDIT:MillardAyo
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!