Wednesday, January 23, 2013

FID Q ATUNUKIWA CHETI MAALUMU NA "UNDER THE SAME SUN"Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma Under The Same Sun kwa mchango wake mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
Ngosha amepost picha akiwa na mwanzilishi na mwenyekiti wa shirika hilo la Canada,Peter Ash, na kuisindikiza picha hiyo na maandishi yanayosomeka "Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and only Mr. Peter Ash (CEO of Under The Same Sun)."Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha watu kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.baada ya miezi kadhaa walirudi tena kanda ya ziwa kuwarudishia shukurani wakaazi wa kanda ya ziwa kwa sababu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yalipungua sana hivyo kampeni yao kwa kushirikiana na wakaazi wa kanda ya ziwa ilifanikiwa.Hongera Fid Q, hard work pays.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!