Monday, January 21, 2013

"SHILOLE HAJITAMBUI...KUTWA NZIMA ANATEMBEA NA WATOTO WADOGO, TENA ANIKOME..!!!!"...BAY MADAHA


KUTOKANA na bifu linalofukuta kama moto wa kifuu kati ya waigizaji, Flora Mvungi na Zuwena Mohamed ‘Shilole’, staa wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameibuka na kumchana Shilole kuwa analitamani Gereza la Segerea.

Akiongea  namwandishi  wetu, Baby Madaha aliyelinunua sakata hilo, alimtaka Shilole kuacha kumfuatafuata shosti wake (Flora) kwani yeye hana lolote zaidi ya kuropoka maneno machafu.


“Eti Shilole anatangaza kuwa atanipiga mimi hebu ajaribu kama yeye mwanamke kweli, mimi haniwezi kamwe. Kwanza hajielewi hata thamani yake, kutwa kutembea na watoto wadogo halafu anajiona staa,” alisema Baby Madaha.
==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!