Wednesday, January 9, 2013

JACK WA CHUZ AIKANA MIMBA YAKE.....


MSANII wa sinema za Kibongo Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’ amekanusha habari zinazosambaa mitaani kwamba ana ujauzito.

Habari hizo zilisambaa baada ya kuonekana picha katika Mtandao wa BBM zikimuonesha  msanii huyo akiwa na kitumbo.

Picha hizo ziliingizwa katika mtandao huo na msanii mwenzake Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye baadaye alithibitisha  kwamba Jack ni mjamzito....

 
 “Kama unavyoniona niko fiti na sina mimba, zile picha tumepiga kwa ajili ya filamu na hakuna kitu kama hicho, wala sitarajii kuwa na mimba kwa siku za hivi karibuni,” alifafanua Jack .

==
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Ubuyu Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Tupe Maoni Yako, Matusi Hapana!